Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imetoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira na kuwakabidhi wanafunzi wa shule za msingi katika kata za Mnamba na Ulumi kupitia bonaza la michezo lililokuwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi na kufanyika katika kijiji cha Ulumi.
Hata hivyo kupitia bonaza hilo kaimu mkuu wa kitengo cha michezo, utamadun na sanaa wilayani humo Amos Mmewa,amesema lengo la michezo hiyo ni kuimarisha afya za wanafunzi na kuibua vipaji vya michezo kupitia wanafunzi na kuwataka maafisa michezo wilayani humo kuhakikisha kila shule inazingatia ratiba za michezo kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata muda wa kufanya mazoezi na michezo mbalimbali kila wiki ili kufikia malengo ya serikali.
Kwa upande wake Mratibu wa michezo wilayani humo James Masoya,amesema licha ya hilo mabonanza hayo yatakuwa endelevu na kwamba wamejipanga kuhakikisha kila tarafa inakuwa na bonaza ambalo litakuwa linashirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo kupitia bonaza hilo timu ya mpira wa miguu wasichana kutoka mnamba iliweza kuibuka na ushindi wa magori mawili dhidi ya timu ya Ulumi, ambapo timu ya Ulumi wavulana iliibuka na ushindi wa gori moja huku timu mpira wa mkono kutoka Mnamba ikiibuka na ushindi wa gori tatu dhidi ya Ulumi ambayo ilipata magori mawili.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.