Uongozi wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa umezindua rasmi ligi ya michezo ya mpira wa miguu maarufu kama ( MISUNGWI CUP) itakayo shirikisha timu 21 kutoka maeneo tofauti ya wilaya hiyo kwa lengo kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kujiajiri wenyewe kupitia michezo.
Akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Afisa tarafa ya Kasanga Andrew Ngindo wakati wa uzinduzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Kateka kata ya Matai, amebainisha kuwa michezo ni ajira michezo ni afya hivyo vijana wanawajibu wa kucheza wakitumainia siku moja kujiajiri wenyewe pamoja na kuimarisha afya zao.
Michezo hiyo inashirikisha timu 21 kutoka kata 23 na vijiji 111 vya wilaya hiyo na mshindi wa kwanza anatarajiwa kutunukiwa mnyama aina ya ng’ombe. Pia michezo hiyo imeandaliwa na mkuu wa wilaya ya kalambo Kalorius Misungwi.
Afisa michezo wilayani humo Amos Mmewa amebainisha kuwa michezo hiyo imekuja katika muda mwafaka ambapo chama cha mpira wa miguu kinatafuta timu ya wilaya ambayo itashiriki katika mashindano ya mkoa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.