• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Kamati ya Amani Rukwa yaandaa siku ya kuliombea Taifa kuwa na uchaguzi wa Aman

Posted on: October 26th, 2020

Katika kuhakikisha uchaguzi mkuu nchini unafanyika kwa utulivu na amani, Kamati ya Amani mkoani Rukwa imeandaa siku maalum kwaajili ya kuliombea taifa kufanikisha uchaguzi huo wa ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 28.10.2020

Wakati akitoa tamko hilo kwa niaba ya kamati, Kaimu Katibu Mtendaji wa kamati hiyo Mchungaji Emanuel Adam Sikazwe wa Kanisa la Monravian alisema kuwa amani ni tunu pekee ambayo watanzania wamepewa na Mwenyezi Mungu na hivyo wana kila sababu ya kuiheshimu, kuilinda na kuitunza ili isitoweke wala kuvunjika.

Aidha, aliwataka vijana kujiepusha na vishawishi vya maandamano, pamoja na kutumika kuanzisha fujo kwani kwa kufanya hivyo mkono wa sheria utawakabili na kutahadharisha kuwa endapo vurugu hizo zikitokea watakaoathirika ni wale wasio na nguvu na wasiojiweza.

“Sisi viongozi wa dini kama wadau wa amani tumekubaliana kuwa na siku maalum ya kufanya maombi kwaajili ya amani kabla ya siku ya uchaguzi ya tarehe 28.10.2020, siku maalum iliyoandaliwa na kamati hii ni siku ya Jumatatu ya tarehe 26.10.2020 na maombi haya pamoja na dua vitafanyika kwenye viwanja vya Sekondari ya Kizwite kuanzia saa tatu asubuhi, hivyo tunawasihi raia wa dini zote kuhudhuria siku hiyo ili kuungana pamoja kumuomba Mwenyezi mungu kuwaleta viongozi waliochaguliwa na kutuondolea ghasia na fujo zitakazoweza kujitokeza siku hiyo ya uchaguzi.”

“Upande wa viongozi wa dini, imebainika kunawatu wanaojitokeza wakiungana na watu wanaohamasisha vijana kufanya fujo ili waweze kuandamana kipindi cha uchaguzi, sisi kama viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa, tunawaomba viongozi wote wa kidini wasijihusishe kabisa na siasa katika kuelekea uchaguzi mkuu.” Alisisitiza

Hayo yamejiri baada ya wajumbe wa kamati hiyo kukutana na kutoa tamko la pamoja kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wote wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi kuzingatia misingi ya sheria na kuheshimu taratibu zilizowekwa katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu Ambele Mwaipopo wa kanisa la KKKT alisisitiza kuwa kamati inatoa tamko hilo kwa nia njema hasa kwa kujali amani nchini tunu ambayo nchi imepewa na Mwenyezi Mungu na wana wajibu wa kuiendeleza wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi ili shughuli za wananchi ziendelee kwa usalama.

Halikadhalika, mmoja wa viongozi wa Taasisi ya Istiqama Mkoani Rukwa Sheikh Ali Baruti alisema kuwa nafasi yao kama viongozi wa dini nchini ni kuendeleza kuhimiza suala la amani na kuongeza kuwa hakuna asiyefahamu umuhimu wa amani kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

“Lazima kuhakikisha watu wanatumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa amani kama ilivyosisitizwa katika Kamati ya Amani ambayo imeundwa na viongozi wetu wa kidini katika mkoa wetu wa Rukwa kwamba watu wote lazima wahakikishe wanakuwa wadau wa kulinda amani na tumesisitiza kwamba suala la haki lazima lilindwe na watu kufuata misingi ya sheria ili kutoleta upenyo wowote ambao unaweza ukawa ni sababu ya kuhamasisha vurugu na kuvunja amani katika nchi yetu,” Alimalizia.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.