Wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameondokana na adha ya kufuata huduma za matibabu katika hospitali ya mkoa iliyopo umbali wa km 50 kutokana na serikali kukamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo iliyojengwa kwa gharama ya shilingi billion 4.4 na kuanza kutoa huduma.
Wakiongea mara baada ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Daniel Chongoro kutembelea hospitali hiyo,wamesema kujengwa kwa hospitali hiyo kumewawezesha kuondoka na adha ya kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma za kibingwa katika hospitali ya mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga na katika nchi jirani ya Zambia.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mganga mkuu wa hosptali hiyo Dkt Emmanuel Mhanda alisema Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi billion 3,440,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa wodi za upasuaji kwa wanawake na wanaume, jengo la kuhifadhia maiti (mortuary), jengo la upasuaji (theatre),jengo la wagonjwa mahututi (ICU) na nyumba ya watumishi na kwamba ujenzi wa wodi tatu ikiwemo wodi ya watoto , wanawake na wanaume zimekamilika na kuanza kutoa huduma.
Awali akiongea na wakazi wa kata za Matai na Lyowa wilayani humo katibu mkuu wa ccm Taifa Daniel Chongolo aliutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kupanda miti ya matunda kuzunguka majengo ya hospitali.
Hata hivyo hospitali ya wilaya ya Wilaya ya Kalambo ina Jumla ya watumishi 50 kati yao madaktari wakiwa 6, wauguzi 24, wataalamu wa maabara 4,katibu1,afisa afya 1, matabibu 4, wafamasia 3, fundi sanifu vifaa tiba 1, tabibu wa meno 1, Mfiziotherapia 1,na wasaidizi wa afya 4.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.