Katibu tawala wilayani kalambo mkoani Rukwa Frank Sichalwe amewaagiza watendaji wa kata kuhakikisha wanagawa vitambulisho vya ujasiliamali kwa wafanyabiashara wote wadogo ili kuwawezesha kuondokana na usumbufu usiokuwa wa lazima.
Akiongea kupitia kikao kazi na watendaji wa kata kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa wilaya hiyo, alisema mpaka sasa fedha zilizoingizwa kwenye mfumo ni shilingi milioni mbili lakisita na themanini (2,680,000) sawa na vitambulisho143 na fedha million 12 .8 sawa na vitambulisho 641.
Alisema lengo la serikali ni kuwawezesha wafanyabishara wadogo kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa na mtu na kuwataka watendaji hao kuhakikisha wanaweka utaratibu maalumu kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji kugawa vitambuliho vya ujasiliamali kwa watendaji wote.
Aidha aliwaagiza maafisa tarafa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji katika uwasilishaji wa vitambulisho na kutoa siku 7 kuhakikisha vitambulisho vyote vinagawiwa kwa watendaji ili viweze kugawiwa kwa wahusika.
Afisa utumishi na utawala wilayani humo Amandus Mtani aliwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kugawa vitambulisho hivyo kwa wajasiliamali ili kuendana na malengo ya serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.