Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu. Gerald M. Kusaya ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi minne aliyokagua katika ziara yake Wilaya ya Kalambo aliyoifanya tarehe 13 Julai 2023. Miradi hiyo yenye thamani zaidi ya Tsh. Bilion 3.04 inatekelezwa kwa fedha za Serikali kuu, fedha za Mradi wa Boost pamoja na mradi Lanes.
Ndugu Kusaya alilidhishwa na hali ya ujenzi baada ya kukagua miradi hiyo ambayo ni mradi wa Shilingi Milion 638.5 (force account) Ujenzi wa shule mpya ya matai B wenye madarasa 16, jengo la utawala pamoja na nyumba ya walimu (2 in 1) Katika Kata ya Lyowa ambapo majengo mengi yapo katika hatua ya renta. Mradi wa Shilingi Milion 109.1 (force account) ujenzi wa madarasa manne shule ya Msingi Kilewani ambapo majengo yapo hatua ya kuezekwa. Mradi wenye majengo sita wa Shilingi Bilion 1.4 Soko la Samaki la Kasanga unaotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya Nice katika Kata ya Kasanga ambapo majengo yapo katika hatua ya renta na kuezeka pamoja na Mradi wa Shilingi Milion 873.2 nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo katika Kata ya Lyowa ikiwa katika hatua ya umaliziaji .
Ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika haraka na kutoa tija kwa wananchi Ndugu Kusaya alitoa maagizo mbalimbali katika ziara hiyo ikiwa ni pamoja na wakandarasi na mafundi kuongeza nguvu ya ujenzi kwa kuongeza mafundi pamoja na kufanya ujenzi usiku na mchana pale inapobidi. Wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya unaotekelezwa na Kampuni ya ujenzi ya Suma JKT, Katibu Tawala Mkoa alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Shafi K. Mpenda kuandaa eneo la ujenzi wa Ikulu ndogo ikiwa ni maandalizi ya awali.
Kukamirika kwa miradi ya ujenzi wa shule na madarasa kutasaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi katika shule husika hali itakayoboresha mazingira ya kijifunzia. Huku ujenzi wa Soko la Samaki la Kasanga ukisaidia kurejesha uhakika wa soko na uifadhi wa Samaki wanaovuliwa katika eneo hilo kufuatia Soko la awali kuzingilwa na Maji ya ziwa Tanganyika.
Aidha Katibu Tawala aliwataka watumishi kutekeleza majukumu yao ipasavyo licha ya uwepo wa madeni mbalimbali wanayoidai Serikali ambapo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuyalipa madeni hayo kadri fedha zinavyopatikana. Hayo aliyasema wakati wa Kikao na watumishi wa Halmashauri waliopo Makao makuu ya Wilaya kabla ya kuanza ziara yake.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala na timu yake kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa waliambatana na mwenyeji wao Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Shafi K. Mpenda, Katibu Tawala Wilaya Ndugu Servi Ndumbaro pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Mradi wa Ujenzi Soko la Samaki Kasanga- Katibu Tawala Mwenye Koti la Suti ya draft.
Mradi Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya
Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya Matai B
Mradi wa Ujenzi wa Madarasa manne Shule ya Msingi Kilewani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.