Hatimaye kaya 210 zilizokuwa zimeathirika kutokana na ongezeko la maji ya ziwa Tanganyika katika kijiji cha Kipwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa zimeondokana na adha ya kulala chini baada ya serikali kwa ushirikiano na mashirika binafsi kutoa misaada ya kibinadamu.
Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Nehemia Mbembela ambaye ni kaimu afisa tarafa ya Kasanga,aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo (Water mission na Save the Children) na kusisistiza kuitumia misaada hiyo kwa kuwasaidia kupunguza makali ya maisha.
‘’naomba pia kutumia fulsa hii kuwaomba kuendelea kushirikiana na wadau wetu kwa kuachangia nguvu kazi ili kukamilisha mradi wa maji kwa wakati. pia ni vizuri tuhakikishe tunatunza miundombinu ya maji ili iweze kuendelea na kutusaidia kwa muda mrefu.’’ Alisema mkuu wa wilaya.
Kwa upande wake meneja wa Shirika la Save the Children Benny Ngereza, alisema shirika hilo limetoa misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, Blanketi pamoja na vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
‘’shirika la Save the children baada ya kubainisha mahitaji ya dharula waliamua kutafuta wadau wenza ili kuhakikisha juhudi za pamoja zinaleta matunda yaliokusudiwa ikiwemo kutoa misaada ya kibinadamu’’ alisema Ngereza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.