Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza bendera zote nchini Uganda kupeperushwa nusu mlingoti kuanzia siku ya Ijumaa, baada ya kifo cha rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kutangazwa usiku wa Jumatano.
Uganda inaungana na mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika mashariki kuomboleza kifo cha shujaa na mwanamapinduzi wa Afrika .
Katika taarifa iliyotolewa kwenye television ya taifa ya Uganda, UBC rais Museveni ametoa salamu za rambirambi kwa wananchi wa Tanzania kwa kupoteza shujaa wa Afrika kwa wakati ambao alikuwa anahitajika zaidi.
Rais Museveni amesema amepata mshutuko mkubwa siku ya Jumatano kutangazwa kifo cha Magufuli na makamu wake wa rais Mama Samia kwamba amefariki baada ya kuuguwa kwa kipindi kifupi, hivyo Uganda na wananchi wa Tanzania wanaungana wakati huu mgumu kwa maombolezo ya kitaifa:
Kabla ya kutoa agizo hilo, rais Museveni alitoa salamu za rambirambi katika mtandao wake wa kijamii, pia amempongeza hayati John Pombe Magufuli kwa utendaji wake tangu kuingia madarakani mwaka 2015.
Hayati John Pombe Magufuli amefariki akiwa ameacha mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka wilayani Hoima nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga Tanzania wa kusafirisha mafuta ya Uganda, ikiwa viongozi wa mataifa hayo mawili walitarajiwa kusaini wiki ijayo ili kuanza rasmi ujenzi wa bomba hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.