Kikao cha baraza la madiwani robo ya tatu 2017 kilichofanyika tarehe 27/04/2017 katika ukumbi wa chuo cha maketekista, Kateka kimejadiri mambo mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi mwaka wa fedha 2016/17.
Katika kikao hicho kilichojadili agenda mbalimbali ambapo agenda ya mapato na matumizi ilitawala kikao hicho hasa katika suala la ukusanyaji mapato huku mvutano ukiwa ni kukusanya mapato kwa kutumia mawakala au kutumia watendaji wa kata na vijiji.
Mvutano huo ulimalizika kwa wajumbe kukubaliana ukusanyaji wa mapato ufanywe na mawakala kwa kipindi cha miezi mitatu ili kupima ufanisi wa ukusanyaji kati ya mawakala hao na ule ukusanyaji wa awali uliokua ukifanywa na watendaji wa kata na vijiji ili kuona ni hupi utafaa kuendelea nao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.