Wizara ya mifugo na uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB imesaini mkataba wa mkopo wa boti ya uvuvi na zana za uvuvi kwa kikundi cha uvuvi cha Umoja kilichopo katika kata ya Samazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa kama hatua ya kuwawezesha wavuvi kujikwamua kiuchumi.
Akiongea ofisini kwake wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo,mkurugenzi mtendaji Halmshauri ya Kalambo Shafi Mpenda, amesema mkopo huo una thamani ya shilingi million thelathini na saba na kwamba umetolewa kwa ajili ya ununuzi wa boti aina ya Fiber, nyavu , mashine na kifaa cha kutafutia samaki ziwani.
Licha ya hilo Mpenda aliipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suruhu hassani kwa kutoa mkopo huo pamoja na boti mbili zenye thamani ya shilingi million 108 ambazo kwa pamoja zinaenda kusaidia kudhibiti uvuvi haramu, udhibiti na usimamizi wa rasilimali uvuvi katika kata za Kasanga na Samazi katika mwambao wa ziwa Tanganyika
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kasanga wilayani humo John Mbita amesema uwepo wa boti hizo unaenda kusaidia wavuvi kunufaika kiuchumi na kuipongeza serikali kwa hatua hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.