Kangi Lugola anakumbukwa kwa misimamo yake akiwa bungeni, halikadhalika baada ya uteuzi wake alibuni vazi la kipekee lenye nembo ya bendera ya Tanzania kwenye mifuko na mikononi na alikuwa akizunguka kila mahali akiwa amebeba kitabu cha ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kangi atakumbukwa kwa uwezo wake wa ushawishi akitumia mbinu ya kuchekesha ili mradi tu hoja yake iungwe mkono.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola atakumbukwa kwa vituko vyake vingi hasa anapokuwa ndani ya bunge na hata nje anapokuwa akitekeleza majukumu yake, akijiita Ninja, yaani shujaa wa kusimamia anayoyaamini.
Miongoni mwa vituko vilivyotia fora ni pamoja na tukio la mwaka jana ambapo alishindwa kujizuia na kuamua kwenda kuungana na Bendi ya polisi nchini Tanzania kusakata muziki na kuonyesha naye ni mjuzi wa kucheza hali iliyoibua shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria shughuli ya ufunguzi wa nyumba za polisi Geita, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
Kuanza kazi kwa kishindo
Bwana Lugola aliingia kwenye majukumu hayo mapya kwa kishindo. Aliteuliwa ukiwa ni mchakato wa mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli.
Mabadiliko hayo yalitangazwa huku Rais Magufuli akieleza pamoja na mambo mengine kutoridhishwa na namna ambavyo suala la ajali za mara kwa mara linavyoshughulikiwa, watu kutowajibika kutokana na matukio hayo.
Lugola alionekana mwiba kutokana na maamuzi na kauli zake dhidi ya viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya mambo ya ndani.
Tamko la kwanza
Mara tu baada ya kuapishwa, Julai 3 mwaka 2020 alifanya ziara mkoani Mbeya kwa lengo la kufanya uchunguzi wa sababu za kukithiri kwa ajali za barabarani kwenye mkoa huo.
Lugola aliagiza kuvunjwa kwa Balaza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na kamati zake zote nchi nzima.
Alisema kuwa aliamua kufanya hivyo kutokana na kushindwa kupambana na ajali.
"Nilikuwa namuuliza mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nikabaini hajui hata sheria inayoliweka baraza hilo na hata kanuni zake hazijui, hii inaonyesha hatuna baraza na kuanzia sasa kwa mamlaka niliyonayo nalivunja baraza hili na nitaliunda upya,". Alisema Lugola.
Tamko la pili
Bwana Kangi Lugola, alimpa maagizo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, akihoji kwanini mabasi hayatembei usiku huku biashara mbalimbali zinafungwa saa 12 jioni.
"IGP aje aniambie mabasi kutotembea usiku ni kwa sababu Jeshi la Polisi limenyoosha mikono kwa majambazi, biashara mbalimbali ikifika saa 12 watu wanafunga wanakwenda majumbani ukiwauliza wanasema ni kwa sababu za usalama, hatuwezi tukakubali kupewa amri na majambazi ni masaa mangapi tufanye shughuli za kiuchumi''.
Tamko la tatu
Lugola: Watanzania ndio waliotulazimu kuweka masharti ya kuondoka nchini
Julai 6, mwaka mwaka jana, Waziri huyo wakati akizungumza na vyombo vya habari pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalana na idara zilizo chini ya wizara hiyo alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwashusha vyeo, Mkuu wa Usalama Barabarani Mbeya, Mrakibu wa Polisi, na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, George Mrutu ambaye alikuwa tayari ameshaenguliwa katika nafasi hiyo.
"Hivyo lazima nichukue hatua kali ili kunusuru maisha ya watu kwani Rais amechoka kutuma salamu za rambirambi,".
Tamko la nne
Katika mkutano huo pia aliwaagiza wakuu wa vyombo vya usalama chini ya wizara yake, kubeba Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa wanafanya kazi ya chama kilichopo madarakani, hivyo ni lazima waitumie katika kuweka mipango kazi.
Tamko la tano
Waziri huyo alitembelea Idara ya Uhamiaji na kuzungumza na watendaji wakuu wa idara hiyo huku akiagiza na kuwataka askari wa uhamiaji waliopo mipakani kujitafakari kwa maelezo kuwa utendaji wao hauridhishi.
''Tatizo liko wapi, inakuaje magari yaliyobeba wahamiaji yanatokea mpaka wa Himo (Kilimanjaro), yanapita Arusha na Manyara, yanakwenda kukamatwa Dodoma?'',Uhamiaji mnakuwa wapi? Inasikitisha watu hawa wanapita mikoa hiyo bila kukamatwa.Watu wa mipakani wajitafakari hatuwezi kukubali hali hii''.
Tamko la sita
Wakati waziri huyo akikagua mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya kupinga usafirishaji wa binadamu papo hapo alimwondoa, Inspekta wa Polisi Kitengo cha Uhamiaji, Abubakar Yunusi katika ujumbe wa Sekretarieti ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu.
Sababu iliyozalisha uamuzi huo ni afisa huyo wa Polisi kutoajua takwimu za vyombo vilivyotumika kusafirisha binadamu ambavyo vimekamatwa na vinasubiri kutaifishwa.
"Wewe umejitambulisha kuwa ni mjumbe wa kamati ya kudhibiti usafirishwaji haramu wa binadamu, umesema kuna vyombo vimetumika, huna idadi yake. Unafanya kazi ya ubabaishaji hapa? Huwezi kuja kwenye maonyesho hujui idadi yake. Kazi yako ya ujumbe hakuna."
Tamko la saba
Baada ya Lugola baada ya kubaini kuwa mbwa maalum wa kikosi cha bandari hayupo mahala pake pa kazi alitoa agizo kwa IGP Sirro akimtaka afuatilia alipo mbwa huyo na kumpa ripoti katika muda ambao ulikuwa hauzidi saa 10.
"Nimesikitishwa kwa kitendo cha mbwa huyu mmoja mpaka sasa haonekani namaelezo niliyopewa hayajaniridhisha kwa sababu kwenye kitabu haijulikani huyumbwa jana alivyotoka alikwenda wapi na alilala wapi na leo haijulikani yupo wapi,kwetu sisi mbwa ni askari," alisema na kuongeza:"Namwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kwamba nitakapomaliza ziara yangumajira ya saa 12:00 anipigie simu akiwa na huyo mbwa pale polisi Bandari ilimwenyewe niweze kufika pale na kumwona huyo mbwa ambaye ni askari."
"Ifikapo saa 12:00 jioni IGP lazima awe na huyu mbwa anionyeshe ili nijiridhishealikuwa wapi na alikuwa amekwenda kufanya nini," alisema.
Tamko la Nane
Lugola aliagiza jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanajilisha na kulisha mahabusu, na kwamba hataki kuona wafungwa nchini wanaishi kama ndege wa angani.
Alisema wafungwa hawalimi ila wanakula bure, badala yake wanatakiwa wafanye kazi na kujitafutia chakula wao wenyewe badala ya kusubiri kupewa chakula na Serikali.
Aliyesema hayo Julai 16 mwaka jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Tuambie kilichorushwa na kituo cha televisheni ya taifa, TBC 1 na kueleza kuwa amewaagiza wasaidizi wake kupitia sheria vizuri na kumpelekea mpango mzuri wa utekelezaji wa agizo la Rais, la kuwatumia wafungwa kufanya kazi za kilimo na ufugaji na kujitafutia chakula wao wenyewe.
"Hata kama ni meno, lazima walimie meno, watatumia meno yao kulima mahindi, kulima maharage ili wajilishe, na nimemwambia Inspekta Jenerali wa Magereza, katika hili sitaki kisingizio cha aina yoyote".
Tamko la tisa
Julai 23, mwaka huu, Waziri huyo aliagiza kuwekwa Mahabusu kwa Askari Polisi aliyekuwa katika kituo cha polisi cha utalii na Diplomasia baada ya kushindwa kuelezea vitabu muhimu vinavyotakiwa kuwa kwenye chumba cha mashitaka.
"Nimeingia kwenye chumba cha mashtaka, nikamkuta askari nikamuuliza vitabu muhimu kwenye chumba hicho akabaki ameduwaa, nikamuagiza RPC (Kamanda wa Polisi) amuweke ndani. Lakini baadaye nikaamuru atolewe kwani yawezekana askari huyo hana elimu ya masuala ya utalii,"
Waziri Lugola alikuwa akikosolewa kwa kiasi kikubwa na wapinzani mbalimbali pia wanasheria kuhusu amri na maagizo ambayo alikuwaa akiyatoa kwa watendaji mbalimbali wa serikali, huku wengine wakikosoa uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kumteua Lugola baada ya kumuweka kando Mwigulu Nchemba huku weengine wakiona hakuna mabadiliko makubwa ya kutarajiwa kutoka kwake.
Kuvuliwa uwaziri
Rais Magufuli alionesha kusikitishwa na utendaji wa viongozi wa wizara ya mambo ya ndani hasa utiaji saini wa mkataba wa 'hovyo' mradi wa thamani ya Euro milioni 408.
Hapo Jana aliamua kutengua uteuzi wa Kangi Lugola na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.