Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola ameliagiza jeshi la polisi mkoani Rukwa kuwasaka,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wabakaji wanne wanaodaiwa kutenda kosa hilo kwa wanafunzi wa shule kisha kukimbilia nchi jirani ya Zambia na kutoa siku saba agizo hilo liwe limetekelezwa.
Ameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matai Wilayani Kalambo mkoani Rukwa, ambapo amesema jeshi la Polisi liko imara na linafanya kazi usiku na mchana hivyo haliwezi kushindwa kuwakamata wabakaji wanaokimbilia kwenye nchi jirani ya Zambia na kokote kule baada ya kufanya uhalifu.
‘’Watoto hawa lazima walindwe, wabakaji hawawezi kulishinda jeshi la Polisi. Natoa siku saba wote wawe wameishakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na taarifa hiyo niipate haraka.’’Amesema lugola huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Aidha, amewataka maredeva wa magari na bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani hususani wakati wa kuendesha vyombo vya moto. Vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa pamoja na kunyang’anywa leseni.
Wananchi kwa upande wao, wameiomba serikali kufungua kituo cha zima moto kwa lengo la kurahisha upatikanaji wa huduma hiyo pindi majanga ya moto yanapotokea. Hivi sasa huduma hiyo inapatikana Manispaa ya Sumbawanga umbali takribani kilometa 52, kutoka Mji wa Matai ambao ndio makao makuu ya Wilaya ya Kalambo.
Aidha wamempongeza mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura pamoja na uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia shuguli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya pamoja na hospital ya wilaya.
‘’kusema kweli mmetuletea mkuu wa wilaya ambae ni mchapa kazi kwani japo kuwa ni mama lakini anachapa kazi kama mwanaume’’walisema wananchi hao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.