Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanzisha utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa bajeti ambayo yatawawezesha kuandaa mpango na bajeti wenye tija na utakao endana na hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Akiongea kupitia kikao cha kuwajengea uwezo wataalamu wa bajeti, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Shafi Mpenda, amesema lengo ni kuwawezesha wataalamu kuwa na uwezo wa kundaa bajeti zinazotekelezeka ,uhalisia na shirikishi.
‘’Mpango na bajeti ni nyezo kuu ya utekelezaji wa dira na mikakati ya maendeleo ya Taifa, Mashirika, pamoja na Taasisi binafsi kwani bila mpango Madhubuti na bajeti inayotekezeka hata ndoto nzuri hubaki kwenye karatasi.’’alisema Mpenda.
Aidha aliwataka kuutumia ujuzi watakao upata kuutumia katika kuongeza chachu ya kuhakikisha rasilimali chache zinakuwa kwenye mpango na kutumika kwa tija, uwazi na uwajibikaji na kusisiza elimu hiyo kuwafikia wataalamu wote hadi ngazi ya Vijiji na Kata.
Hata hivyo mafunzo hayo yanajumuisha wakuu vitengo na Divisheni pamoja na wataalamu wa bajeti kwa ngazi ya Halmashauri.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.