Mkutano wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa umewapiga marufuku wafanyabishara wote kusafirisha mizigo ya mazao nyakati za usiku ikiwa ni jitihada za kudhibiti upotevu wa fedha za mapato na kumtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Msongera Paela, kuhakikisha anaweka migambo kwenye mageti yote sambamba na kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya fedha kutoka kwa watendaji wa vijiji.
Halmashauri ya wilaya ya kalambo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 ilikuwa na makisio ya kukusanya fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani kiasi cha shilingi bilion mbili na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja nukuta mbili sawa na asilimia 61.05.
Awali wakiongea kupitia kikao cha baraza la madiwani wilayani humo, wamesema kwa mwaka 2019 na 2020 wameazimia kufikia malengo ya ukusanyaji mapato kwa kushirikina na watendaji wa vijiji na kata na kumshauri mkurugenzi mtendaji kutowaruhusu watendaji kukaa na fedha za makusanyo kwa muda mrefu.
Mkurugezi mtendaji wa halmashauri hiyo Msongera Palela ,amesema wamejipanga kubuni vyanzo vipya vya mapato nakuwasihi madiwani kutoa ushirikiano katika zoezi zima la ukusanyaji mapato.
‘’Tumejidhatiti kuanzisha zoezi la kutoa hati za ardhi za kimila na leseni za makazi kwa wananchi pamoja na kutoa elimu juu ya manufaa ya mpango huo ili Halmashauri ipige hatua mbele’’alisema msongela.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe, amesema ofisi ya mkuu wa wilaya itaendelea kuwasaka na kuwachukulia hatua watendaji wote ambao washindwa kufanya marejesho ya fedha za mapato kwa muda muafaka.
‘’ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugezni mtendaji wa halmashauri itaendelea kuwasaka na kuwachukulia hatua waatendaji ambao wagundulika kukaa na fedha majumbani kama ilivyo fanya kwa mwaka wa fedha uliopita’’ alisema sichalwe.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.