Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka 2020 imefanikiwa kusajili mashauri 176 na kumaliza mashauri 197 huku mahakama za mwanzo zikifanikiwa kusajili mashauri 349 na kumaliza mashauri 369.
Mahakama kuu nchini Tanzania ilitambuliwa na katiba ya Jamhuri ya mungano wa Tanzania mwaka 1977 na badae kuanzishwa kwa mahakama ya lufani mwaka 1979. Akiongea jana wakati wa kilele cha madhimisho ya miaka 100 ya mahakama nchini ,Hakimu mkazi mwandamizi wa wilaya ya Kalambo Ramadhani Lugemalila ,alisema tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu nchini, serikali imefainikiwa kuanzisha masijala kuu ya Mahakama ya Tanzania na kanda za mahakama kuu 16 na Divisheni za mahakama kuu 4 ambazo ni pamoja na Aridhi, Biashara, kazi na Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi.
Alisema ibara ya 107 (1) ya katiba ya jamhuri ya mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inazitaka mahakama zote nchini kutoa haki kwa wananchi wote bila kujali hali ya mtu, kijamii au kiuchumi na kusema utoaji wa haki unatakiwa kutolewa kwa wakati sambamba na kutoa fidia kwa waathirika na makosa ya watu wengine ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza usuruhushi wa migogoro.
Aidha alisema kwa kutekeleza hilo mahakama ya wilaya ya Kalambo kwa mwaka 2020 iliweza kusajili mashauri 176 na kufanikiwa kumaliza mashauri 197 na kubakiza mashauri 32.
Alisema licha ya hilo katika mahakama za mwanzo walifanikiwa kusajili mashauri 349 na kumaliza mashauri 369 na mashauri 16 yakibakia na kusema kwa idadi hiyo mahakama ziliweza kufikia malengo yake yaliowekwa na mahakama ya Tanzania.
‘’vile vile kila hakimu kulingana na ngazi zao pamoja na waheshimiwa majaji wamewekewa kiwango maalumu cha mashauri ya kusikiliza na kuyamaliza ndani ya mwaka husika. kwa mahakimu waliopo mahakama za mwanzo wanatakiwa kumaliza kesi 260 na mahikimu waliopo mahakama za wilaya na mahakama za hakimu mkazi wanatakiwa kumaliza kesi 250 na waheshimiwa majaji wao wanalazimika kumaliza kesi 220. Alisema lugemalila.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.