...Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Ndg. Frank Sichalwe kwa niaba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, akisisitiza jambo alipokua akihutubia wananchi waliojitokeza katika maonesho ya Nanenane ngazi ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo yaliyofanyika Tarehe 26 hadi 27 Julai 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daud Sichone, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika (DAICO) Ndg. Nicholous Mrango.
Wilaya ya Kalambo inatarajia kushiriki katika maonesho ya Nanenane katika ngazi ya Kanda ya Nyanda za Juu Mkoani Mbeya, yatakayoanza Tarehe 01/08/2017 hadi kilele cha Maonesho hayo Tarehe 08/08/2017. Kupitia Maonesho hayo Wilaya ya Kalambo itaweza Kutangaza vivutio mbalimbali vya kiuchumi na Kiutalii vilivyopo katika Wilaya ikiwa ni pamoja na kubadirishana mbinu bora na Taasisi zingine katika nyanja mbalimbali kama vile kilimo,Ufugaji,Uvuvi,Utalii na kadharika. Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo “Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.