Mashabiki wa timu ya yanga Sc mkoani Rukwa wamejitokeza kufanya usafi katika maeno tofauti ya manispaa ya sumbawanga ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kufaanya usafiki kila jumamosi ya mwisho wa mwezi
Mashabiki hao wamejitokeza kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa rukwa na kuungana na watu wengine katika kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni pamojaa na kujitolea kutoa damu katika baadhi ya hosptali zilizopo mkoani hapa .
Mashabiki hao wamedai kuwa wao kama wanamichezo wanaamini katika usafi na ndiyo maana wamejitokeza kwa wingi kufanya kazi hiyo na kuwa yanga yenyewe imejikita zaidi katika shughuli za kijamii na kuwa hiyo ni moja ya malengo yao.
Riziki Awadi mwanachama wa Yanga amedai kuwa wao kwao imekua ni kawaida kushiriki katika shughuli hizo za kijamii lakini kubwa ni kuunga mkono kauli ya Rais ya kuifanya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya usafi na kuwa ni muhimu kwa kila mtu kufanya usafi
Alisema kuwa si mara yao ya kwanza kufanya hivyo na kuwataka watani wenzao ambao ni Simba kuiga utaratibu huu ambao ni mzuri wa kushiriki shughuli kama hizo za kijamii na kuwa hiyo inaweza kuwa ni njia ya kuwahamasisha na watu wengine kushiriki katika shughuli kama hizo za kijamii.
Asheri Benard kwa upande wake amesema kuwa hilo wanalolifanya sasa ni maandalizi ya kuelekea kwenye siku ya Yanga (Yanga Day ) na wana Imani kuwa siku hiyo watafanya mambo makubwa.
Pia amedai kuwa katika mpango wao watakwenda pia kujitolea damu kwa ajiri ya kuwasaidia watu wengine wenye matatizo yanayohitaji damu hususani Mama wajawazito.
Sambamba na hilo wanachama wa Yanga tawi la Kalambo nao katika kuadhimisha Yanga day wamekwenda katika hospitali ya wilaya ya Kalambo kwa ajili ya kujitolea damu.
Mwisho
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.