• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Mfahamu Waziri Mkuu Wa Tanzania

Posted on: November 12th, 2020

Mfahamu Waziri Mkuu Wa TanzBwana Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye anaendelea na wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa muhula wa pili, alizaliwa tarehe 22 Desemba mwaka 1960 yaani miaka 60 iliyopita.

Kitaaluma ni Mwalimu aliyepata elimu yake ya Ualimu katika chuo cha ualimu cha Mtwara mwaka 1991-1993, na baadae kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden.

Kutoka mwaka 1984 mpaka 2006 amehudumu katika nafasi mbalimbali kama mwalimu na kiongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka 2006 Majaliwa aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya na kisha akajitosa kwenye siasa za ushindani mwaka 2010 alipogombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi.

Baadaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Bw Majaliwa ameidhinishwa kuwa Waziri Mkuu na Bunge baada ya jina lake kuwasilishwa bungeni na mpambe wa rais John Magufuli na kupigiwa kura ya ndiyo na wabunge wote 350 waliokuwepo ukumbini. Anatarajiwa kula kiapo hivi karibuni ili kuanza rasmi majukumu yake.

Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita. Endapo atadumu katika wadhifa huo kwa kipindi chote cha pili cha rais Magufuli atakuwa Waziri Mkuu wa pili kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo. Fredrick Sumaye, ndiye mtu pekee mpaka sasa aliyehudumu kwa miaka 10 mfululizo kama Waziri Mkuu wa Tanzania kutoka mwaka 1995 mpaka 2005 chini ya rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa

Uteuzi wa Majaliwa hii leo haukusthua wengi kama alivyoteuliwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita. Wachambuzi wengi walitarajia Majaliwa kurejea katika nafasi yake, mosi kutokana na kauli ya rais Magufuli na pili kutokana na utendaji wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli alizungumza wakati wa tukio la kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, kwamba viongozi wa serikali hawatakiwi kuwa na hofu ya nafasi zao kwa sababu mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita yalitokana na ufanisi wao pia.

Ingawa alisema kutakuwa na mabadiliko makubwa katika baraza jipya la mawaziri, ni vigumu kutenganisha mafanikio ya utawala wa Awamu ya Tano na utendaji wa Waziri Mkuu. Katika mawaziri wote wa serikali ya Rais Magufuli, Majaliwa - kama kiranja wa mawaziri wengine, ndiye pekee ambaye nafasi yake inafungamanishwa moja kwa moja na Rais katika utendaji.

Bw Majaliwa anatokea kusini mwa Tanzania eneo ambalo mtu wa mwisho kutoka ukanda huo kuwa waziri mkuu alikuwa Mzee Rashid Kawawa aliyekuwa Waziri Mkuu miaka ya mwanzoni ya uhuru. Yeye nimtu wa 11 kuwa Waziri Mkuu tangu Tanganyika ilipopata uhuru ambapo Waziri Mkuu wa kwanza alikuwa Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa kila siku wa kazi na shughuli za Serikali, atakuwa na madaraka ya kuongoza shughuli za serikali Bungeni.

Atakuwa na madaraka ya kutekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo rais ataagiza yatekelezwe.

Pia Waziri Mkuu atakuwa na madaraka ya kumshauri rais kuhusu uteuzi wa Mawaziri.

Anayo madaraka ya kumshauri rais kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri.

Waziri Mkuu huyu ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu, na pia amesomea ualimu wa mpira. Katika kipindi cha mwaka 2010-2015 alikuwa Kocha wa timu ya soka inayoundwa na wabunge.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.