Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ametatua mgogoro sugu wa ardhi katika kijiji cha Ilimba kata ya Mkoe wilaya ya Kalambo kwa kumwagiza kamishina wa ardhi mkoani humo kutoa hekali 100 kati ya hekali 634 zilizokuwa zilikimilikiwa na mwekezaji na kurejeshwa kwa wananchi kwa kukimilikisha kijiji na kutoa hati miliki.
Kwa mujibu wa wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo wamedai kuwa mgogoro wa ardhi baina yao na mwekezaji ulijitokeza kufuatia mwekezaji kuongezewa muda wa umiliki wa eneo hilo kinyume na utaratibu. Ambapo kutokana na hali hiyo mkuu wa mkoa huo Makongoro Nyerere ameingilia kati swala hilo na kuuagiza uongozi wa wilaya hiyo kutafuta eneo la wazi kisha kulipima na kutoa hati miliki kwa wananchi na kusema mwekezaji anamiliki eneo hilo kihalali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.