Katika jitihada za kutekeleza afua za lishe kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano mkoani Rukwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imetenga jumla ya shilingi milioni sitini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Sereman Jafo [MB] kutenga fedha kiasi cha shilingi elfu moja kwa kila mtoto ili kupambana na udumavu na utapia mlo unaokadiriwa kuwa asilimia 56.3 Mkoani hapa.
Akiongea na kamati za lishe Kaimu Mkurugezi Mtendaji Wilayani humo Eriki Kayombo, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kama sehemu ya Mkoa wa Rukwa haipaswi kuwa na ulemavu kutokana na uzalishaji mkubwa wa chakula na huduma bora za jamii zikiwemo Afya,Usafirishaji na utawala bora kwa Wananchi.
Pamoja na maelezo hayo, Kaimu Mkurugenzi Kayombo amezitaka shule za Msingi na Sekondari Wilayani Kalambo kuyaendeleza mashamba yote ya shule ili kuzalisha chakula na kuanza kukitoa kwa Wanafunzi wote hasa wakati wa mchana kwa wale wa kutwa wakati Serikali ikiendelea na huduma hiyo kwa watoto wa bweni.
‘’Lazima watoto wote wapate chakula katika shule zote kwa maana ya Msingi na Sekondari ili tuondokane na udumavu hii ni aibu kwetu jamani,’’Anasisitiza Kayombo.
Sanjali na hayo, amewataka Wakuu wa shule katika ngazi zote kuendelea kusimamia utoaji taaluma bora ili Wilaya iendelee kung’ara akitolea mfano wa matokeo mazuri yaliyopatikana katika mitihani ya Moko kidato cha nne mwaka huu ambapo Wilaya imeshika nafasi ya pili kimkoa, kwani kati ya wanafunzi 983 waliotahiniwa, 792 wamefaulu sawa na asilimia 80.6 ikilinganishwa na asilimia 65 ya mwaka 2018 ambapo Wilaya ilichukua nafasi ya nne.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.