Wanafunzi katika shule ya Sekondari wasichana Kalambo mkoani Rukwa wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya bwalo na bweni baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi 155,219.891.95 kisha kuanza ujenzi ambao umefikia asilimia 98 ya ukamilishaji.
Mkuu wa shule hiyo Felista Sichula amebainisha kuwa serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi 56,331,491.91 kwa ajili ya umaliziaji wa bweni na shilingi 98,884,000 ikiwa ni kwa ajili ya umaliziaji wa Bwalo na kwamba uwepo wa miradi hiyo utawezesha wanafunzi kuishi katika mazingira rafiki na kupunguza utoro na mimba za utotoni.
‘’Tunatoa shukrani za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya umaliziaji wa miundombinu ya shule ambayo itawezesha wanafunzi kukaa katika sehemu rafiki’’
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ametembelea miradi hiyo na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kwa utekelezaji mzuri wa miradi hiyo na kuwataka wanafunzi kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.