Mwenge wa uhuru wilayani Kalambo mkoani Rukwa umezindua na,kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 7 yenye thamani ya shilingi 3,065, 853,014.83 na kukimbizwa umbali wa km 227 katika vijiji 14 vya wilaya hiyo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Shaibu Kaim amezindua mradi wa wanafunzi wenye mahitaji maalmu katika kijiji cha Msanzi wenye thamani ya shillingi 110,000,000,.00, klabu ya wapinga Rushwa, katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kalambo, ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2023 ikiwa na idadi ya wanachama 80.
Licha ya hilo mwenge wa uhuru umezindua Klabu ya kuzuia matumizi ya dawa za kulevya katika shule ya Sekondari ya wasichana Kalambo ikiwa na idadi ya wasichana 52.
Aidha kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa amezindua mradi wa zahanati ya kijiji cha Mbuza kata ya mkoe ambao uliibuniwa na wananchi baada ya zahanati iliopo kuwa ndogo huku idadi ya wananchi wanao pata matibabu ikiwa ni kubwa na kughalimu kiasi cha shilingi 154,128,260 na kuupongeza uongozi wa Halmshauri ya Kalambo kwa kujenga jengo hilo kwa kiwango.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.