Wajumbe wa kamati ya Mwenge wa Uhuru wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuweka utaratibu maalumu ambao utasaidia kuwawajibisha kisheria viongozi ambao wamekuwa wakisababisha kukataliwa kwa miradi ya maendeleo na viongozi wa mbio za mwenge kitaifa na kuisababishia serikali hasara.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2021 unatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa madarasa mawili ya Msanzi Sekondari, Uzinduzi wa mradi wa maji kijiji cha Singiwe, ukaguzi wa Klabu ya Maralia na Ukumwi, ukaguzi wa kikundi cha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, pamoja na ujenzi wa jiwe la msingi Zahanati ya Mbuza.
Kwa mujibu wa mratibu wa maandalizi ya mwenge wa uhuru wilayani humo Ibrahim Mwanauta, alisema mwenge wa uhuru utakagua na kuzindua miradi katika maeneo ya kasanga, Matai na Msanzi, ambapo kwa kata ya Kasanga utakagua mradi wa CTC, Klabu ya Lishe, upokeaji hundi kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, kupokea taarifa ya mabanda mbalimbali katika eneo la Matai.
Mkurugezni mtendaji wa Hamashauri hiyo Msongea Palela, alisema mkesha wa mwenge wa uhuru utafanyika katika eneo la Matai na kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge mara utakapo wasili na kupita kwenye maeneo yao husika.
Awali akiongea kupitia kwenye kikao hicho mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela, alisema hato sita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya viongozi ambao watasababisha kukataliwa kwa miradi ya maendeleo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.