Wakati tukielekea madhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani ,mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewataka wataalamu wa afya mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa unyonyeshaji kwa akina mama wote kwa lengo la kusaidia kupata watoto wenye ulewa na afya nzuri.
Wiki ya unyonyeshaji hufanyika kuanzia tarehe moja ya kuanzia agosti moja hadi saba kila mwaka,ambapo kwa mwaka 2019 madhimisho hayo kimkoa yatafanyika katika kata ya kisusumba wilayani kalambo na huku kauli mbiu ikiwa ni ‘’mwezeshe mama aweze kunyonyesha’’
Akiongea ofisini kwake mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema lengo la serikali ni kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusu jinsi,usawa wa kijinsia,sheria na kanuni zinavyowezesha kulinda ,kuendeleza na kusaidia uonyeshaji maziwa ya mama ili kuboresha lishe ya watoto na jamii.
‘’unyonyeshaji ni jukumu la kila mtu katika nafasi yake,watu hao ni pamoja na baba,familia,viongozi ngazi ya jaamii,wafaanyakazi wa afya wenye ujuzi ,wataamu wa masuala ya uonyonyeshaji na marafiki, pia ni vizuri kwa mama kupata muda na msaada wa kutosha katika kipindi cha kunyonyesha na pia apate elimu ya makuzi na malezi kwa watoto wake’’alisema Wangabo.
Alisema licha ya hilo vyombo vya habari vinaweza kufuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazolinda haki za uzazi na uzalishaji wa watoto kwa kufanya tafiti,kuandika,kuripoti matukio mbalimbali ikiwemo haki ya kupata likizo ya uzazi.
Kaimu afisa lishe mkoani humo Asha Izina, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha akina mama wote wanapewa kipaumbele zaidi hususani wakati wa kipindi cha unyonyeshaji kwa lengo la kusaidia kuondokana na adha ya udumavu kwa watoto
Madhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yatafanyika sambamba na siku ya afya ya kijiji yatakayo fanyika katika vijiji vyote kuanzia agost moja 2019 katika kijiji cha Kisumbakati wilayani kalambo mkoani hapa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.