Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwela amesema maandalizi kwa ajili ya ziara ya kutembelea kivutio cha utalii cha maporomoko ya maji ya Kalambo yamekamilika na kuwa sasa yatafanyika tarehe 18 Desemba mwaka huu lengo ikiwa kukuza utalii wa ndani ya Mkoa wa Rukwa .
Mwela ametoa taarifa hiyo leo mjini Sumbawanga alipoongea na wanahabari na kubainisha kuwa
‘’Ikumbukwe Kalambo water Falls Ni Mapolomoko ya Pili kwa ukubwa kutoka Yale ya Afrika kusini.Pia ina vivutio vya misitu ya Asili,Hifadhi na Maeneo ambayo yanavutia kiutalii.Yapo maeneo ya kuweka makambi kwa ajili ya kuchoma Nyama,ngoma,Kuogelea, Jogging na Burudani mbalimbali huku ukilitazama jua la kuzama kwa uzuri(Sun set) kupitia ziwa Tanganyika,ziwa lililojaa Samaki wenye Radha ya kipekee barani Afrika.Maji yake meupe yenye kukuwezesha kuona kina kwa chini na kukupa urahisi Kuogelea.Tembelea maeneo hayo usiishie tu kusimuliwa’’ alisema Mwela.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.