Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt Lazaro amelipongeza shirika la PLAN INTERNATIONAL kwa kushirikiana na serikali katika kujenga uwezo na kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa shule za msingi na awali tangu kuanza kwa mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni mwaka 2020.
Ameyasema hayo kupitia hafla ya kufunga na kukabidhi shughuli za mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni 2020-2024 uliokuwa ukitekelezwa katika wilaya ya Nkasi ,Sumbawanga vijijini na Kalambo na kuzitaka idara husika wilayani humo kuziimarisha kamati za MTAKUWA kuanzia ngazi za vijiji ili ziweze kuwa sehemu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
‘’nashukuru tena PLAN INTERNATIONAL kwa kunialika na kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kulinda haki za watoto, nawashukuru na kuwapongeza tena viongozi na wafanyakazi wote wa mashirika wenza na sisi kama serikali tuendelee kuwaunga mkono katika juhudi hizi’’alisema Dkt Komba.
Kaimu mkurugenzi wa miradi ya PLAN INTERNATIONAL nchini Tanzania Laurent James Wambura amesema tangu kuanza kwa mradi huo kamati 152 katika vijiji 116 za MTAKUWA zilianzishwa na kuimarishwa na kwamba kamati hizo zipo katika hatua mbalimbali za kuidhinishwa kwenye mkoa wa Rukwa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mtoto.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.