...Mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo umeenza utekelezaji wake ambapo kwa sasa ujenzi huo upo katika hatua ya ujenzi wa msingi. Jengo hilo litakua na vyumba vya ofisi takribani 60 ambavyo vitatumiwa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kalambo ambapo pia ofisi zingine zitakodishwa kwa taasisi mbalimbali zenye uhitaji. Mbali na vyumba vya ofisi jengo hilo litakua na ukumbi wa Mikutano, sehemu ya chakula n.k
Ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 20 hasa ikiwa fedha za ujenzi wa jengo hilo zitakua zikifika kwa wakati kutoka Serikali kuu. Kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kutoa nafasi ya kufunguliwa kwa shule ya wasichana Matai shule ambayo kwa sasa majengo yake yanatumika kama ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauli ya Wilaya ya Kalambo. Ufunguzi wa shule hiyo utapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba wa shule za sekondari unaoikabiri Wilaya ya Kalambo.
Mbali na ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ujenzi wa majengo ya taasisi mbalimbali za serikali umekua ukiendelea katika Wilaya ya Kalambo ambapo majengo ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Tanesco, VETA yamekua yakiendelea kujengwa kwa kasi ya hali ya juu. Sambamba na ujenzi wa majengo ya taasisi ujenzi wa nyumba bora za makazi umeendelea kushika hatamu katika maeneo mbalimbali ambayo yamepimwa katika mji wa Matai na kuufanya Mji huo kuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi.
Mji wa Matai unatarajiwa kuwa kituo kikuu cha biashara kati ya nchi ya Tanzania na nchi jirani ya Zambia pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika kwa barabara zinazounganisha nchi hizo katika kiwango cha rami pamoja na uboreshaji wa bandari ya Kasanga.
Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Ujenzi wa nyumba bora za makazi katika Mji wa Matai
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.