Msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Shafi Mpenda ametangaza rasmi uwepo wa uchaguzi wa serikali za mitaa November 27/2024 na kuwataka wadau wa uchaguzi kuyafikia makundi yote ya kijamii ikiwemo watu wenye hali ya ulemavu kwa kutoa elimu juu ya ushiriki wao kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ameyasema hayo kupitia kikao kilicho jumuisha wadau wa uchaguzi wilayani humo wakiwemo watendaji wa kata na vijiji na kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuchagua viongozi bora watakao waongoza.
‘’wa mujibu wa Tangazo la uchaguzi lililotolewa kwa kuzingatia kanuni ya 4 ya Kanuni za uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Tangazo la Serikali Na. 571, uchaguzi utafanyika tarehe 27 Novemba 2024 na Kwa mujibu wa Kanuni ya 11 (GN. Na. 571/Mamlaka za Wilaya, zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024 katika vituo vilivyopangwa’’ alisema Mpenda.
Aidha alitoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo kuanzia hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. Kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwani ni hatua muhimu inayompa kila mwananchi mwenye sifa haki ya kisheria kushiriki uchaguzi kama mpiga kura au mgombea.
‘’ikiwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ,2024, na kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (1), na (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Ngazi ya Vijiji na Vitongoji katika Mamlaka za Wilaya Nimepewa Mamlaka ya kutoa Maelekezo ya namna uchaguzi huu utakavyofanyika’’
Alisema maelekezo hayo yanafafanua hatua zitakazoongoza mchakato wa uchaguzi, kuanzia uandikishaji wa wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea, uteuzi wa wagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi. Maelekezo haya yanalenga kutoa mwongozo ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na usawa na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.