• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Msimu Mpya Wa Kilimo Kuzinduliwa Rasmi Mkoani Rukwa.

Posted on: November 24th, 2020

Wakati mvua zikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, wakulima wa Mkoa wa Rukwa wameshuhudia uzinduzi wa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 katika hafla fupi iliyofanyika katika Kata ya Ntendo, Manispaa ya Sumbawanga.

Uzinduzi huo uliofanywa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wauzaji wa zana za kilimo, mbolea, mbegu na miche ya mazao ya Korosho na mibuni ambayo ni mazao kimkakati katika mkoa.

Wakati akiwahutubia wananchi waliohudhuria uzinduzi huo Mh. Wangabo alisema kuwa mkoa umepania kuongeza hekta za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao hasa zao la Mahindi ambalo ndio zao kuu la chakula na biashara katika mkoa akitoa msukumo katika kilimo cha mazao mengine ya kimakati yakiwemo Alizeti, Kahawa, Korosho na Michikichi yatakayongeza wigo wa mazao ya kibiashara.

“Kati ya eneo litakalo limwa katika msimu wa mwaka 2020/2021, jumla ya hekta 483,380.63 ni kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na hekta 58,797.04 ni kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara. Aidha, Jumla ya tani 1,568,067.67 za mazao zinategemewa kuzalishwa. Ambapo tani 1,464,140.63 ni za mazao ya chakula na tani 103,927.04 za mazao ya biashara. Malengo ya uzalishaji ya mwaka huu ni sawa na ongezeko la asilimia 22 ya uzalishaji wa mwaka uliopita wa 2019/2020”

“Katika msimu wa 2020/2021 jumla ya hekta 100.8 zinatarajiwa kupandwa miche ya Kahawa 252,000. Aidha, kwa upande wa Alizeti Mkoa unalenga kulima hekta 52,371.9 ambazo zitazalisha tani 60,205.88 na katika msimu wa Mwaka 2020/2021 Mkoa umeagiza kiasi cha tani 3.5 za mbegu ya korosho kutoka Bodi ya Korosho Tanzania ambazo zitaoteshwa kwenye vitalu. Kiasi hicho cha mbegu kitatosha kupanda eneo la ekari 125.” Alisema.

 

Kwa upande wake Mrajis wa vyama vya ushirika mkoa wa Rukwa Benjamin Mwangwala akieleza mipango ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania alisema kuwa tume hiyo imeendelea kutekeleza mpango wa kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini kwa kumsaidia mkulima na vyama vya ushirika kuongeza kipato kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji kwa kutumia zana bora za kilimo.

“Vyama vya Ushirika vipatavyo 45 vilifanikiwa kufikia matakwa ya masharti ya kupata mkopo wa matrekta kupitia Mikutano Mikuu ya Vyama vya Ushirika. Miongoni mwa masharti ni pamoja na kuwa na taasisi iliyosajiliwa kisheria, kutoa malipo ya awali ya asilimia 25 ya thamani ya zana hitajika. Aidha, kwa mtu mmoja mmoja ni lazima awe mwanachama wa Chama cha Ushirika,” Alisema.

Aidha aliongeza kuwa Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano wakulima hao wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la kukosa mfuko maalum wa pembejeo jambo linalochangia Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Rukwa kukosa dhamana ya kuagiza mbolea kwa kutumia mfumo wa Uagizaji wa Pamoja kama serikali ilivyoelekeza.

Mahitaji ya Pembejeo za kilimo Mkoani Rukwa kwa msimu wa Mwaka wa 2020/2021 ni tani 26,152 za mbolea ambapo DAP tani 10,164.00, UREA tani 9,402.00, CAN tani 3,044.00, NPK tani 2,143.50 na SA tani 1,398.50.

 S

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.