• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Mtoto Afariki Dunia Na Wengine 30 Kupatiwa Matibabu Baada Ya Kula Mzoga Wa Nguruwe

Posted on: December 28th, 2019

MTOTO Maren Namsukuma (7) amefariki dunia na watu wengine 30 wamepata matibabu  katika zahanati ya Kalembe Kijiji cha Utengule kata ya Mambwe Nkoswe wilayani Kalambo mkoani Rukwa baada ya kula mzoga wa nguruwe.

Kwamujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoani Rukwa Justine Masejo ilisema kuwa siku ya Desemba 21 Osward Simpungwe alichinja nguruwe ambaye alikuwa amekufua mwenyewe na kisha kuanza kuuza nyama.

Wakazi wa kijiji hicho akiwemo baba wa marehemu walinunua nyama hiyo na kuitumia kwaajili ya kitoweo, ndipo waliokula nyama hiyo walianza kuugua ugonjwa ambao haukujulikana mara moja.

Kabla ya kufariki mtoto huyo familia nzima walilalamika kuumwa tumbo, ndipo baba yao alipokwenda kwenye duka la dawa muhimu za binaadamu na kununua Flagyl pamoja na Panadol na kumpatia mtoto huyo,lakini hata hivyo hazikumsaidia na hali yake ilizidi kuwa mbaya na ilipofika majira ya saa 10 usiku siku ya Desemba 25, alifariki dunia wakati wakienda katika zahanati ya Kijiji kupata matibabu.

Mmoja wa wakazi wakazi wa Kijiji hicho aliyenusurika baada ya kula nyama hiyo, Aberi Sinyangwe alisema kuwa katika Kijiji hicho kumekuwa na changamoto ya kutokea matukio hayo kutokana na kukosekana kwa maafisa mifugo ambao wanajukumu la kukagua ubora wa nyama kabla ya kuliwa na binaadamu.

Aliiomba serikali kupeleka wataalamu hao kwa ili waondokane na tatizo la kujirudia kwa matukio hayo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Wigani Namsukuma alisema kuwa baada ya serikali ya kijiji kupata taarifa za tukio hilo ilitoa taarifa polisi na kisha kuwakimbiza katika zahanati ya Kijiji wagonjwa 30 waliougua baada ya kula nyama hiyo na walipatiwa matibabu lakini kwa bahati mbaya alifariki mtoto huyo.

Naye ofisa mifugo wa wilaya ya Kalambo, Enos Luvinga aliwaonya wakazi wa Kijiji hicho kuacha tabia ya kula nyama za mifugo inayo jifia yenyewe kwani ni hatari kwa afya zao kwakua mifugo hiyo inakuwa na magonjwa ndiyo maana inajifia yenyewe.

Kaimu Mganga mkuu was wilaya ya Kalambo Rock Sabuni aliwashauri wakazi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kujinunulia dawa na kutumia bila kupata ushauri wa daktari, badala yake wanapougua wawe wanakwenda haraka katika zahanati na vituo vya afya kwaajili ya matibabu.

Kamanda Masejo alisema kuwa Simpungwe anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kutokana na kosa la kuwauzia watu nyama ya mzoga huo na atafikishwa mahakamani baada ya mahojiano hayo kukamilika.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.