• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Mwalimu Wa Shule Ya Msingi Kisumba Kibindoni Kwa Tuhuma Za Kumpatia Ujauzito Mwanafunzi.

Posted on: December 8th, 2019

Jeshi la polisi wilayani Kalambo mkoani Rukwa inamshikilia mwalimu wa shule ya msingi Kisumba(jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 31 kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Chisenga iliyopo wilayani humo.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa polisi mkoani humo Justine Masejo ilieleza kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 18 alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo hadi kupelekea kumpa ujauzito.

Kamanda Masejo alisema kuwa mpaka sasa mkoani humo kuna jumla ya matukio 27 yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi ambayo yanahusiana na wanafunzi kukatisha masomo baada ya kupewa ujauzito.

Alisema kuwa katika kesi hizo wanafunzi 20 ni wa shule za sekondari na saba ni shule za msingi na zipo katika hatua mbalimbali za upelelezi huku baadhi zimekwisha fikishwa mahakamani.

Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa hivi sasa jeshi hilo la polisi lina endesha operesheni maalum ya kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi na wanafunzi kwani wamekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa nia njema ya serikali ya kutoa elimu bila malipo ili wanafunzi wengi waweze kusoma mkoani Rukwa.

Alisema katika tukio hilo lililotokea hivi karibuni bado polisi wanaendelea na upelelezi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.