Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daud Sichone amewataka Waheshimiwa Madiwani pamoja Wananchi kwa Ujumla kutotafsiri vibaya agizo ya Rais Mh. Dk. John Pombe Magufuli la kutochangia michango katika utekelezaji wa sera ya Elimu bila malipo na kuzitaka Serikali za Vijiji na Kata kuanzisha na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja uchangiaji wa madawati ili kufikia maendeleo katika Halmashauri na Nchi kwa ujumla. Matakwa hayo yalisemwa katika Mkutano wa pili wa Baraza la Madiwani katika Mwaka wa fedha 2017-2018 lililofanyika tarehe 30 Januari 2018 wakati wa kujibu maswali ya papo kwa papo ya Waheshimiwa Madiwani.
Akijibu swali la uhaba wa madawati katika shule mbalimbali lililoulizwa na Diwani wa Kata ya Mkowe Mh. Zozimo, Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Simon C. Ngagani ameeleza kuwa ataendelea kusisitiza na kisimamia mpango ambao uliafikiwa na kupitishwa na Halmashauri ambapo Kata pamoja na Vijiji kuendelea na zoezi la utafutaji mbao na mafundi ambapo Halmashauri itagharamia gharama za Ufundi baada ya utengenezwaji wa Madawati hayo.
Akitoa maelezo ya ziada Afisa Elimu Wilaya ya Kalambo Ephraim Moses amewataka wananchi kupitia Serikali za Vijiji kuanzisha mchakato wa uchangiaji wa madawati ambapo Ofisi ya Mkurugenzi itaomba kibali Ofisi ya Katibu Tawaka Mkoa juu ya kutekeleza shughuri hiyo. Aidha amesisitiza wananchi kutotafsiri vibaya Kauli ya Rais Mh. Dk. John Pombe Magufuli, ambapo amesema kuwa Rais ametakaza michango holela pamoja na suala la urudishaji wa wanafunzi majumbani pale wazazi wanaposhindwa kutoa mchango.
Katika suala la Kuboresha Ukusanyaji wa mapato, Mwenyekiti wa Halmashauri amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuongeza mashine za kukusanyia mapato-PoS ili kila Kijiji kiweze kuwa na mashine hizo na kuwezesha kusanya wa mapato na kuongeza kiwango cha mapato katika Halmashauri.
Wadau mbalimbali, Katika baraza hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini-TARURA Wilaya ya Kalambo, ameeleza namna ambavyo mapendekezo ya changamoto mbalimbali za barabara zinavyoweza kuwafikia kupitia njia rasmi. Amesema kuwa mbali na TARURA kufuatilia changamoto za barabara TARURA inapokea changamoto za Madiwani katika maeneo yao kupitia Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo. Pia Meneja wa Wakala wa Misitu Nchini-TFS Wilaya ya Kalambo alipata nafasi ya kutoa maelezo ya namna Taasisi hiyo inavyoshiriki katika kukuza shughuli mbalimbali za kijamii na utalii katika Wilaya Kalambo ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali za Taasisis hiyo.
Aidha katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ametoa maagizo kwa watendaji wote katika Kata na Vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kusoma taarifa za mapato na matumizi kufikia tarehe 5 Februari mwaka huu ambapo watakaoshindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua. Pia Mkuu wa Wilaya ameagiza kufungwa kwa Ziwa Sundu kwa kipindi cha miezi mitatu (3) na kusimamishwa kwa shughuli zote za uvuvi katika ziwa hilo ili kutoa nafasi ya ukuaji wa samaki pamoja na kuzaliana.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.