• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Naibu Katibu Mkuu Atoa Siku Saba Ujenzi Kituo Cha Afya Samazi Kuanza Kujengwa.

Posted on: January 15th, 2020


WAKAZI wa Kijiji cha Samazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelalamikia kucheleweshwa  kwa ujenzi wa kituo cha afya ambacho kilitakiwa kujengwa tangia june 2019 kutokana na  fedha  kutolewa na serikali  kiasi cha shilingi million 400 na hivyo kuwa na hofu ya fedha hizo kuhamishwa.

Malalamiko hayo waliyatoa mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Dorothy Gwajima alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo na kutembelea eneo linalojengwa kituo hicho cha afya.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho Saimon Kapesa alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa kituo cha afya katika kata yao,wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 20 kutafuta huduma za afya katika kata nyingine hivyo waliiomba serikali iwajengee kutuo hicho cha afya haraka ili kuwaondolea usumbufu.

"Katika Kijiji chetu, tunalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 20 kutafuta huduma za afya, na hii ni tabu zaidi kwa akina mama wajawazito na watoto ambapo wakati mwingine wanahitaji huduma za dharura na pengine hata baadhi ya vifo vinavyotokea kijijini hapa vinatokana na kukosekana kwa matibabu kwa wakati" alisema.

Naye Monica Nakazwe mkazi wa Kijiji hicho alisema kuwa haoni sababu kwanini kuna kusua sua katika ujenzi wa kituo hicho ilihali serikali imekwisha toa fedha kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho kwani kwa kufanya hivyo kunawasababishia usumbufu na gharama zisizokuwa za lazima katika kufuata huduma za afya katika vituo vya afya vya Ngorotwa na Matai, ambavyo vipo mbali na kijiji chao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Nicholaus Mlango alisema kuwa ni kweli serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400 na tayari halmashauri hiyo imekwisha anza ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo, Frank Sichalwe aliishukuru serikali  kwa kutoa fedha hizo ambapo tayari ujenzi wa kituo cha afya umekwisha anza na utakapo kamikika utaondoa kero zinazo wakabili wakazi wa kijiji hicho.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Gwajima alitishia kuzichukua fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 400 zilizotolewa na serikali kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha samazi, huku akimpa siku saba Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Kalambo kuanza mara moja ujenzi wa kituo hicho ambacho umeshindwa kuanza kwa takribani miezi minane kutokana na mvutano wa eneo la ujenzi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.