Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu mhandisi Logatus Mativila amemwagiza meneja wa TARURA mkoani Rukwa kuharakisha ujenzi wa daraja la Mto Kalambo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 67 ili kuwawesha wananchi kunufaika na huduma hiyo haraka.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi daraja la mto huo lililopo wilayani Kalambo Mkoani Rukwa,ambapo amesema daraja hilo linatekelezwa na TARURA makao makuu kupitia fedha za maendeleo kutoka serikali kuu (mfuko wa tozo za mafuta ) na kwamba mradi huo utakapo kamilika utahudumia wakazi wa kata ya Sopa na Mpombwe.
Meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi William Lameck,amesema hadi sasa mkandarasi amelipwa jumla ya shilingi 1,750,293,898.22 ikiwa ni hati ya malipo ya kwanza na kwamba mkataba huo hauna muda wa nyongeza na unatakiwa kukamilika ndani ya muda wa miezi 12.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.