Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Josephati kandege ametoa misaada ya vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuliko yaliosababisha zaidi ya nyumba 138 kubomoka na watu 139 kukosa makazi katika kijiji cha kipwa wilayani kalambo mkoani Rukwa .
Kijiji cha Kipwa kipo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia lakini kwa hivi sasa kijiji hicho kinakabiliwa na kadhia ya maji ya ziwa Tanganyika kuzingira makazi yao .
Maji hayo yamesababisha Zaidi ya nyumba 138 kubomoka na kaya 139 kuacha makazi na huku changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni watu wengi kukosa chakula pamoja na vitu vya kujifunika ikiwemo mablanketi na matenti.
Hali hiyo imepelekea Naibu waziri ofis ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Josephat Kandege kufika kijijini hapo kisha kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa wakazi wa kijiji hicho ikiwemo unga kiasi cha tani moja.
Hata hivyo katika ziara hiyo ametumia fulsa hiyo kuwasihi wananchi wa kijiji hicho kuhakikisha wanahamia katika maeneo ya milima Mawesande ambako maji ya ziwa hilo hayawezi kufika kiurahisi na kulipongeza shirika la msalaba mwekundu kwa kuwezesha mablanketi 100 na magodoro 100 wakazi wa kijiji hicho na kuwa msaada huo ni mkubwa.
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo Endrue Ngindo, amesema licha ya hilo mkoa umetoa kilo 100 za sukari pamoja na matenti 16 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi hao.
Wakazi wa kijiji hicho kwa upande wao wamesema msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa na kuwasihi watu wengine kuendelea kufika maeneo hayo ili kuwasaidia.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.