Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania na waziri wa nishati Dkt,Dotto Biteko ameweka jiwe jiwe la msingi njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania (TAZA) pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tangameda,Kisada,Iganjo, Nkangamo na Malangali.
Mradi huu umelenga kuunganisha mkoa wa Rukwa na grid ya Taifa ikiwa ni pamoja na kuunganisha na mataifa mengine ya Afrika ili kuwa na umeme wa uhakika kwa asilimia 100.
Dkt.Biteko, amesema mkoa wa Rukwa haujaunganishwa na Grid ya taifa toka Nchi ipate uhuru na kuwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ni kutaka kuona mkoa Rukwa na mikoa mingine yote nchini Tanzania inaunganishwa kwenye gridi ya taifa ili kuwa na umeme wa uhakika na watu waweze kuutumia umeme katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uzalishaji mali.
Alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kwa mkoa Rukwa kuingizwa kwenye gridi ya Taifa na kuwa licha ya kwamba Rukwa inategemea umeme kutoka Zambia sasa watautumia umem wa ndani na kuwa wataendelea kuungana na Zambia ambao utakua unatumika pale Tanzania inapotokea hitilafu na kwamba hali hiyo itawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika wakati wote na kumtaka mkandarasi kuhakikisha anautekeleza mradi huo kwa haraka.
Awali katibu mkuu wa wizara ya nishati Mhandisi Felchwan Mramba, alisema kuwa mradi huo ni wa kipekee utakaowezesha afrika kuunganishwa na umeme kutoka Afrika kusini hadi Ethiopia na kuwa Tanzania itakuwa na umeme wa uhakika na kuwavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza kutokana na uhakika wa umeme nchini.
Alidai kuwa wao kama wizara watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kubwa ni kuona changamoto hiyo ya umeme inatoweka Nchini na kuwa katika mpango wa serikali wa kuhakikisha mashine zote za kufua umeme hasa katika bwawa la walimu Nyerere zinafanya kazi na kuwa sasa umeme ni mwingi hadi baadhi ya mashine nyingine wameamua kuzizima hivyo hari ya umeme nchini ni nzuri.
Mkurugenzi wa Tanesco Gissima Nyamohanga, amesema kuwa wao kama shirika kupitia mradi huo wa (TAZA) ilikua ni kuziunganisha nchi tatu ambazo ni kenya,Tanzania na Zambia na kuunganishwa na nchi 13 za Afrika na kuwa hilo litasaidia mataifa haya kuuziana umeme kiurahisi pale inapotokea nchi moja inapopata hitilafu na kuwa sasa Afrika nzima umeme utakua ni wa uhakika.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere alimpongeza Mhe,Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan kupitia wizara hiyo kwa namna ambavyo wameamua kuondoa tatizo la umeme nchini hasa mkoa Rukwa na kwamba klukamilika kwake kutavutia wawekezaji wengi kuwekeza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.