Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisem Josephat kandege ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kuhakikisha mradi wa maji wa Myunga unakamilika kabla ya june 30,2019 na kutishia kumfutia lesen mkandas wa mradi huo endapo ataenda kinyume na mkataba utavyo taka.
Mradi wa maji wa Myunga ulinza kujengwa novembar 2017 na huku ukitakiwa kukamilika julai 31 2018 na ukijumuisha ufungaji wa umeme wa sola sambamba na kujenga vituo 20 vya maji kwa gharama ya zaidi ya shilingi million 630.
Awali akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa idara ya maji wilayani humo ENG Bakar Kiwitu ,amesema mradi huo upo kwenye asilimia sitini 60% za utekelezaji.
‘’Kazi zilizo fanyika ni pamoja na mabomba yenye vipenyo mbalimbali vyenye jumla ya urefu wa kilometa zote 7.698 yamelazwa,ujenzi wa vituo 2 kati ya 20 vya kuchotea maji ,ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 150,000 umefikia asilimia 75.’’alisema kiwitu.
Kwa upande wake Naibu waziri wa nchi ofis ya Rais Tamisem Josephat kandege alisema endapo mradi huo ukikamilika utawanufaisha wananchi kwenye vijiji kumi na kuutaka uongozi husika kuhakikisha unasimamia kwa ukaribu ili mradi huo uweze kukamilika kwa haraka.
‘’kampuni hii endapo itashindwa kutekeleza mradi huu kwa wakati itakuwa miongoni mwa kampuni ambazo hazitapewa tenda tena na serikali hivyo nisingependa kuona hali kama hii ikijitokeza hivyo nina imani kufikia june 30 ,2019 mradi huu uwe umekamirikali tayari kwa matumizi’’.alisema kandege.
Hata hivyo mpaka sasa mkandaras emelipwa kias cha shilingi million 148.8 sawa na aslimia 23 na huku changamoto kubwa inayokwamisha kukamilishwa kwa mradi huo ikitajwa kuwa ni mkandasi kufanya kazi kwa kasi ndogo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.