Benki ya NMB imefanikiwa kupunguza uhaba wa madawati katika shule ya sekondari Ulungu na Matai kwa kutoa msaada wa meza Mia moja 100 na viti hamsini (50) vyenye thamani ya shilingi milioni kumi (10,000,000/=) ambavyo vitasaidia kupunguza kero ya wanafunzi kukaa chini na kurahisha zoezi la ujifunzaji na ufundishaji.
Akiongea kwa niaba ya walimu wa shule hizo mkuu wa shule ya Ulungu Jackson Kaulu ambae licha ya kuipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ,amesema licha ya hilo shule hizo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitanda kwa upande wa hosteli ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za maji.
Awali akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo afisa elimu sekondari wilayani humo Ramadhan Mabula ambae licha ya kuipongeza benki hiyo kwa kutoa msaada huo akasisitiza wadau kuendelea kujitokeza kwani shule nyingi bado zina uhitaji wa meza, viti na vifaa vya michezo
‘’tunaomba muendelee kutusaidia vitu mbalimbali kwani bado tuna uhitaji mkubwa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.Pia tunaomba msaada wa pampu za maji ili kutatua chanagamoto ya kukatika kwa maji ‘’alisema Mabula.
Mwenyewkiti wa halmashauri hiyo Daudi Sichone ametumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao ili kufikia malengo yao ya baadae kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika uboreshaji wa miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.