MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa zimeendelea kusababisha maafa kwa baadhi ya maeneo huku mtu mmoja akifariki dunia na nyumba saba kuanguka katika wilaya ya Kalambo .
Katika tukio la kwanza limetokea katika kijiji cha Kanyarakata kata ya Mbuluma, ambapo mkazi mmoja wa kijiji hicho alifariki dunia wakati akivusha mifugo yake kwenye mto Kalambo na kusombwa na maji na kukutwa akiwa amefariki dunia.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliwasihi wananchi wilayani humo kuwamakini hususani katika kipindi hiki cha masika.
‘’wananchi wanatakiwa kuwa makini hususani wakati wa kuvuka kwenye mito kwani mvua ni nyingi na zinaweza kusababisha matatizo dhidi yao kama ilivyotokea katika kata ya Mbuluma’’. alisema Binyura.
Katika tukio lingine limetokea katika kijiji cha kasanga ambako nyumba saba zimeanguka kufuatia mvua kubwa ilionyesha katika maaeneo hayo.
Afisa tarafa hiyo Endrue Manyema Ngindo , amesema chanzo ni kutokana na mto Katete kuhama njia na kupeleka maji yake katika makazi ya watu na hivyo kusababisha baadhi ya nyumba kuanguka.
Alisemaa licha ya hilo mvua hiyo ilisababisha maafa katika kijiji cha Kipwa na kupelekea familia moja kukosa makazi.
Hata hivyo siku za hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alitembelea maeneo ya bonde la ziwa Rukwa kufuatia maafa ya mvua kutokea katika vijiji vya Kinambo, Maenje, Milepa, Sakalilo na Talanda vilivyopo kata ya Milepa na Ilemba, katika bonde la Ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga, ambako Zaidi ya nyumba 135 zilibomoka na kaya 72 kukosa makazi .
Katika salamu zake Mh. Wangabo alisema kuwa janga hilo hakuna aliyelitegemea na kulifananisha tukio hilo na ajali ambayo haina kinga na ndio sababu iliyopelekea kufika hapo kutoa pole kutokana na janga hilo na kuwapongeza wale waliowahifadhi ndugu na jamaa ambao wamekosa mahala pa kuishi kutokana na nyumba zao kuangushwa na mvua hiyo.
Aidha, katika ziara yake hiyo alitoa kilo 500 za unga wa sembe pamoja na kilo 200 za maharage kwa kamati ya maafa ya wilaya ili waweze kugawa kwa waathiriwa wa mvua hiyo katika vijiji hivyo vya bonde la Ziwa Rukwa na kuwataka wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kusaidia waathiriwa hao ili waweze kurudi katika maisha yao ya kawaida.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.