Mkuu wa kituo cha polisi Matai ASP Hassan Nkindwa amezindua rasmi mashindano ya ligi ya mpira wa miguu yanayofahamika kama DKT SITIMA MATAI OPEN SCHOOL yanayoshirikisha timu 18 kutoka kata 23 za halmashauri ya wilaya ya Kalambo na kuwataka vijana kuyatumia mashindano hayo katika kuibua vipaji na kuimarisha afya
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya,mkuu wa kituo hicho Hassan Nkinda amesema michezo hiyo ina lengo la kuibua vipaji vya vijana pamoja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto wakiwemo madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda na madereva wa bajaji.
Mapema akiongea na wadau wa michezo wilayani humo mwenyekiti wa mashindano hayo Kalos Mbalazi amesema mshindi wa kwanza atajipatia fedha kiasi cha shilingi laki tatu (300000/=) mshindi wa pili atajipatia shilingi laki mbili (200000/=) na mshindi wa tatu atajipatia shilingi laki moja (100000/=) na kwamba wachezaji bora na walinda lango (goalkeeper) watazawadiwa fedha kiasi cha shilingi elfu ishirini (20000/=).
Kaimu Afisa michezo wilayani humo James Masoya aliwataka wadau kuendelea kujitokeza kudhamini kwenye michezo ili kupata vijana wengi zaidi wenye uwezo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.