Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Philip Isdory Mpango kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya Jumanne na mpambe wa Rais katika bahasha maalum.
Baada ya kupokea Spika Job Ndugai alilitangazia bunge hilo jina hilo lililopendekezwa na rais Samia.
Mara baada ya tangazo hilo bunge lililipuka kwa shangwe.
Bwana Mpango amekuwa waziri mwandamizi katika serikali ya hayati John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha.
Kwa sasa, bunge la Tanzania linatarajiwa kupiga kura ili kuthibitisha uteuzi huo wa Mpango.
Na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, asilimia 50 ya wabunge wanatakiwa kuukubali uteuzi huo ili kuthibitishwa.
Kabla ya jina hilo kuwasilishwa bungeni hii leo, kwanza liliwasilishwa katika Kamati kuu ya chama tawala CCM na kuthibitishwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.