Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo K. Pinda amewataka wananchi kulima zao la Karanga miti (Makadamia) ili kujiinua kiuchumi. Mh. Pinda ameyasema hayo jijini Mbeya alipotembelea banda ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo katika Maonesho ya Kilimo ya Mwaka 2023 maarufu kama Maonesho ya Nanenane.
Jamani limeni zao la Makadamia, hili zao la Makadamia halipunguzi umaskini tu, bali linatajirisha kabisa. Mh. Pinda aliyasema maneno hayo alipokuwa akitizama bidhaa za taasisi ya Grace Community Development and Education ambaye mdau wa kilimo katika Wilaya ya Kalambo. Baada ya kutembelea banda hilo aliipongeza Kalambo kwa kuanzisha kilimo cha zao hilo ambalo kilo moja ya karanga Tanzania kwa sasa ni Tzs 40,000 hadi 60,000. Mh. Pinda aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Makongoro Nyerere.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo anaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda hilo ili kujionea bidhaa bora za kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazopatika katika Wilaya ya Kalambo, ikiwa ni pamoja kujifunza mbinu bora za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Maonesho ya Nanenane 2023, Nyanda za Juu Kusini yanaendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya yakiwa na kaulimbiu, Vijana na Wanawake ni Msingi wa Mifumo Endelevu ya Chakula. Maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan tarehe 08 Agosti 2023.
Miche ya Makadamia
Mh.Pinda akidadisi jambo kuhusu chakula na lishe.
Mh. Pinda katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.