Baada ya kuapishwa urais katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma nchini Tanzani.
Rais huyo ametoa shukrani kwa watanzania wote kumuamini na kumchagua kwa mara nyingine kuliongoza taifa hilo kwa miaka mingine mitano.
Katika hotuba yake amesisitiza kuwa ushindi aliopata sio wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM) bali ni ushindi kwa Watanzania wote.
"Ushindi huu ni wa Watanzania wote. Nawapongeza sana Watanzania kwa kuonyesha utulivu mkubwa katika kipindi chote cha uchaguzi. Tumepita kwenye mitihani mingi lakini mara zote Mungu ametuvusha salama" Magufuli amesema.
Pia ameipongeza Tume ya uchaguzi Tanzania (NEC) kwa kusimamia vyema uchaguzi huo.
Aidha, Bwana Magufuli amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwavusha katika janga la corona.
Rais John Magufuli amesisitiza kwamba sasa uchaguzi umekwisha na kuwa jukumu kubwa ni kuendeleza jitihada za kuleta maendeleo katika taifa hilo.
"Nitashirikiana nanyi nyote bila kujali itikadi na utofauti wetu" Magufuli amesema.
"Tutazidisha mapambano dhidi ya rushwa, wizi na ubadhirifu" Magufuli ameongeza.
Amemshukuru Mungu kwa fursa ya yeye kuwa rais wa kwanza kuapishwa katika jiji la Dodoma.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.