Rais wa Tanzania John Magufuli hii leo amemuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa awamu ya pili Prof Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dkt Philip Mpango Waziri wa fedha na mipango.
Watatu hao wameapishwa leo mjini Dodoma, huku Rais Magufuli akieleza sababu za mchakato wa kuunda baraza la mawaziri kuwa wa polepole kuliko ilivyotarajiwa na wengi.
Rais Magufuli amesema hana haraka sana ya kuteua baraza la mawaziri.
"Mwaka huu, tuna wabunge zaidi ya 350 na bado wabunge wa nafasi zile kumi wa mimi kuteua, sikutaka niteue haraka haraka. Mwaka 2015 ilikuwa rahisi kwasababu idadi ya wabunge wa CCM ilikuwa ndogo''
Masuala ya fedha na Diplomasia ni muhimu
Dkt Magufuli ameeleza umuhimu wa kuwa na Waziri wa fedha kwa kuwa zinahitajika na kwamba haziwezi kusubiri kwa miezi mitatu..minne
''Si kwamba hawa wawili ni maarufu sana kuliko waliobaki, miaka ya nyuma niliwateua hawakuwa na majimbo, na niliwaambia waende kwenye majimbo au waende huko walikotoka, wakaenda kwenye majimbo.'' Alisema Magufuli
''Lakini kwa sababu niliona kuwa nitachelewa kidogo kuwa na baraza la mawaziri na ninyi waheshimiwa wabunge lazima mlipwe mishahara na posho zenu na lazima tutafue fedha za kulipa mishahara wafanyakazi na watanzania na lazima tuendelee kuwa na miradi ya maji na barabara ambayo haisimami'' Alisema.
Rais Magufuli amemsifu Dkt Mpango kutokana na jitihada zake katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati
"Kabla ya kutumikia miaka mitano ya kwanza alikuwa kamishna wa TRA , alikuwa mtu wa kwanza kukusanya mapato kutoka 850 bilioni hadi trilioni 1.2.
"Kwenye wizara ya mambo ya nje, hatuwezi kukosa mtu wa kutusemea", alisema Rais Magufuli
"Tukaendelea kutukanwa watu wanatengeneza majambo yao hayapati majibu kwasababu nchi yetu haiwezi kuishi katika hali ya kujitenga ndio maana nikasema huyu kwa sababu alimudu kazi yake ngoja aendelee kuwa Waziri wa mambo ya nje.''
Wapo wengi waliomudu nafasi zao lakini Rais Magufuli amesema ameona ajiridhishe kwanza.
''Wasaidizi wangu walishaniletea ushauri, unajua Wizara ya ulinzi na Wizara ya Mambo ya ndani napo ungefanya hivyo hivyo wala sikuwajibu kwasababu si lazima uwe na waziri wa ulinzi''.
Ukihitaji polisi wakafanye kazi zao wakafanye kazi mahali popote wala hauhitaji waziri wa mambo ya ndani, IGP atafoka tu kule watu watamsikiliza.
Rais Magufuli ameeleza kuwa ni Waziri Mkuu mmoja tu Fredrick Sumaye (1995-2005) ambaye amedumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na wengine wote walikaa kwa vipi fi vifupi zaidi.kwa upande wake, baada ya kula kiapi katika ya Ikulu Chamwino, Waziri mkuu Majaliwa amesema,
''Nakushukuru sana rais kwa kunipa nafasi tena, Mh. Rais utaunda Baraza la Mawaziri muda mfupi ujao jukumu langu ni kusimamia utendaji kazi wao, nitapita kila wizara na kuwataka waweke mpango kazi wa yale yaliyoanzishwa kwenye Ilani na kwenye hotuba yako''.
Majaliwa ameonesha atakayoyapa kipaumbele ikiwemo kupanda kwa bei ya saruji na kuahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo.''Tulipokuwa kwenye kampeni, kumeibuka kupanda kwa bei ya saruji bila sababu ya msingi, hatutarajii saruji kuwa na bei kubwa...sasa naanza na hili la saruji'', Amesema Bwana Majaaliwa.
Dkt. Philip Mpango waziri wa fedha naye amemshukuru Mungu kwa makuu aliyomtendea na kuahidi utendaji uliotukuka.
''Ingawa tupo kwenye uchumi wa kati, huko nilikokwenda kwenye Kampeni umasikini bado ni mkubwa, tunahitaji kuwatumikia watu wetu, ninaamini rais ukiwa kwenye kiti chako inawezekana Tanzania ikawa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati ila kwa kiwango cha juu'', Bwana Mpango alisema.
''Kwa hiyo wizara nyingine zote zitasimama ili nijiridhishe'' alisema Magufuli. Amesema kuwa atakaa na viongozi wenzake wa juu ili kutekeleza jukumu hilo.
Rais Magufuli amemsifu Majaliwa akisema ni mchapakazi na muadilifu na anastahili nafasi hiyo, japo si sahihi kwa watu kuhesabu kuwa atasalia kwa kipindi chote cha miaka mitano.
"Baada tu ya kumchagua kuwa Waziri Mkuu naona kuna watu wanasherehekea na baadhi ya magazeti yanaandika kuwa atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10. Hilo si sahihi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.