Ndege ya Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada imeachiliwa, rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli ameeleza.
Bila kusema imeachiwa lini, na kwa makubaliano gani, rais Magufuli amewaambia wananchi mkoani Mwanza wajiandae kuipokea mkoani hapo.
Ndege aina ya Bombardier Q400 ilikamatwa nchni Canada baada ya mkulima mstaafa Hermanus Steyn kuishtaki serikali ya Tanzania nchini humo.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa mkulima huyo kufungua malalamishi ambayo yalisababisha ndege za Tanzania kushikiliwa.
Mwezi Agosti, Steyn alifungua Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini katika jimbo la Gauteng akidai fidia ya dola 33 milioni.
Mkulima huyo anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980.
Sahauri hilo lilisababisha Mahakama hiyo ya Gauteng kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo.
Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimshinda mkulima huyo mahakamani hapo mpaka katika ngazi ya rufaa na hatimaye Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo kuachiliwa.
Novemba 23, 2019, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi alitangaza kushikiliwa kwa Bombardier Q400 nchini Caanada, "ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini."
Serikali ya Tanzania ilituma wanasheria wake nchini humo, na pia kufanya mazungumzo na balozi wa Canada nchini Tanzania.
Rais Magufuli jana alitoa tangazo la kuachiliwa ndege hiyo wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama tawala cha CCM jana Alhamisi Desemba 12, jijini Mwanza: "ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiliwa, wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokea na tutaipokelea hapa Mwanza."
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.