Rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania Mhe .Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Rukwa kuanzia tarehe 15 hadi 17 Julai 2024 kwa kuzindua miradi 10 ya maendeleo ikiwa ni mara yake ya kwanza ya kutembelea mkoa wa Rukwa tangu aapishwe kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere akiwa ofisini kwake amesema Mh. Rais atazindua hosptali ya Wilaya ya Nkasi, barabara ya Sumbawanga – Kasanga, chuo cha ualimu Sumbwanga, chuo cha Veta cha Sumbawanga, ujenzi wa ghala/vihenge vya kuhifadhia nafaka (NFRA) Sumbawanga na uzinduzi wa jengo la utawala la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Kalambo.
Aidha amesema licha ya hayo Mh.Rais pia ataweka mawe ya msingi katika miradi mitano ikiwemo mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Sumbawanga, Jengo la chuo cha MUST, Barabara ya kiwango cha lami ya Kaengesa, na ujenzi wa shule ya wasichana ya Laela (Rukwa Girls) na baadae kufanya mkutano mkuu wa hadhara na wananchi katika uwanja wa Nelson Mandela katika manispaa ya sumbawanga.
Hata hivyo Mh.Rais kwa mara ya mwisho alitembelea mkoa wa Rukwa mwaka 2020 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais ,wabunge na madiwani, wakati huo Mh.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania na mgombea Mwenza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.