Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewataka wananchi Mkoani humo kujitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27/2024 na kuvitaka vyama vya siasa kusimamisha wagombea wanao kubalika na jamii ili kupata viongozi bora na ambao wataleta tija katika jamii na taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kisumba Wilayani Kalambo Mkoani humo na kusisistiza jamii kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi wanao wataka.
Licha ya hilo alitumia fursa hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya hiyo kuwarejesha kwenye nafasi zao wagombea ambao waliondolewa kwenye nafasi zao baada ya kugundulika kuwa na makosa madogo madogo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.