Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Makongoro Nyerere ameelezea kufurahishwa na kitendo cha uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo kwa kuanzisha mpango wa matumizi wa unga lishe wa Samaki kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwani utasaidia kukabiliana na tatizo la udumavu na utapia mlo mkali kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Ameyasema hayo wakati wa ukagauzi wa mabanda ya maonesho ya wakulima ambayo yanafanyika kwa nyanda za juu kusjini jijini Mbeya na kuitaka jamii kuzingatia matumizi ya vyakula bora na vyenye virutubishi kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kuyatumia maonesho hayo katika kujifunza mbinu bora za kilimo,ufugaji na uvuvi
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.