Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere amewaonya wenyeviti wa serikali za vijiji vya Samazi na Kisala wilayani Kalambo baada ya kubainika kuwashawishi Wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Kata inayoendelea kujengwa katika kijiji cha Kipanga.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo na kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Dkt. Lazaro Komba kukaa kikao na viongozi wa vijiji hivyo ili kuruhusu wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Alisema atawawajibisha viongozi wote wa serikali za vijiji ambao wataendelea kuwa na msimamo wa kutotoa ushirikiano katika ujenzi wa mradi wa shule hiyo na kusisitiza wananchi kuungana kwani kujigawa ni kukwamisha jitahada za serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
‘’Salamu yetu ni kuungana, tukijigawa hatuna nguvu, na kama anae fanya hivyo ni kiongozi wa serikali ya kijiji, tunandikia andiko linakuja kwangu, linakwenda kwa Waziri tunafanya uchaguzi mwingine.lakini Wananchi wajue kwanza kwanini tunamtoa aliepo madarakani .Alisema Makongoro.
Hata hivyo shule mpya ya Samazi ilipokea kiasi cha shilingi milion 583,180,028,kutoka SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa majengo 26 ikiwemo madarasa 8, maabara 3, jengo la utawala 1, matundu 12 ya vyoo, jengo moja la Tehama na Maktaba.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.