• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

RC SONGWE AIPONGEZA HALMSHAURI YA KALAMBO KWA UBUNIFU

Posted on: August 6th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel  Chongoro ameipongeza Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa kuanzisha teknolojia mpya ya ukaushaji wa dagaa na samaki  kwa kutumia kaushio la kisasa (solar tent drier) ambalo litawezesha upatikanaji  wa samaki  na dagaa wenye ubora na kuwezesha wavuvi kujikwamua na hali ya kiuchumi.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupitia maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika kikanda Jijini Mbeya na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya Kalambo kwa kuanzisha teknolojia hiyo ambayo itaweszeha kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvuliwa hususani kipindi cha masika.

Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda ,Afisa uvuvi wilayani humo  Bw. Abdul Balozi ,Amesema sambamba na teknolojia hiyo pia wameleta bidhaa mpya ya unga wa samaki  ambayo ni ya kwanza kwa kanda ya nyanda za juu kusini ambayo itasaidia kupunguza udumavu na utapia mlo kwa watoto kutokana na unga huo kuwa na virutubisho vyote.

‘’Unga huu utaweza kutumiwa na watu wote ikiwemo watoto wachanga,na watu wazima na katika kuhakikisha huduma hii inapatika sehemu zote za mwambao wa ziwa Tanganyika kwa kushirikina na mradi wa FISH4ACP tumejenga makaushio makubwa matatu na jiko moja la kubanikia samaki katika vijiji vya Kasanga, Kilewani na Samazi’’,alisema  Bw. Balozi.  

Kwa upande wake mkuu wa Divisheni ya kilimo , mifugo na uvuvi Bw. Nicholas Mrango amesema licha ya hilo Halmshauri imetenga fedha milion sitini na moja ( 61,000,000/=) kwa ajili ya  utekelezaji wa afua za lishe ikiwemo kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya vyakula bora kwa lengo la kutokomeza tatizo la udumavu wilayani humo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA KALAMBO YAFIKIA ASILIMIA 120 UKUSANYAJI WA MAPATO.

    June 27, 2025
  • HALMASHAURI YA KALAMBO YAFIKIA ASILIMIA 120 UKUSANYAJI WA MAPATO.

    June 27, 2025
  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.